YESU SI MUNGUNI MTUME WA MUNGU
1. "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."
Yohana 17 : 3
2. "Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani."
Yohana 5 :24
3. "Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka."
Yohana 5 : 30
4. "Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona."
Yohana 5 : 37
5. "Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Yohana 6 : 38
6. "Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka.
Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.
Yohana 7 : 16 - 18
7. " Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.
Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
Yohana 7 : 28 ĺ 29
8. "Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.
Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.
Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini.
Yohana 8 : 28 - 30
9. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Yohana 11 : 39 - 44
10. "Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka."
Yohana 12 : 44
11. "Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo."
Yohana 12 :49 - 50
12. "Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka."
Yohana 14 : 24
13. "Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi."
Yohana 14 : 28
14. "Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako.
Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma."
Yohana 17 : 6 - 8
15. " Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu."
Yohana 20 : 17
16. "Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake."
Yohana 4 : 34
17. "Tena, mtu mkubwa mmoja alimwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?
Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu."
Luka 18 : 18 - 19
18. "Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha ?"
Matayo 27 : 46
19. "Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
Luka 6 : 12
20. "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba."
Matayo 24 : 26; Marko 13 : 32
21. "Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote."
1 Wakorintho 15 : 28
22. "Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa."
Luka 4 : 43 - 44
23. " Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.
Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando."
Luka 7 : 16 - 17
24. "Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?
Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya."
Matayo 21 : 10 - 11
25. "Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni."
Yohana 6 : 14
26. "Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii."
Yohana 9 : 17
27. "Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;"
1 Timotheo 2 : 5
28. "Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;" Waefeso 1 : 17
isaya 9:6
Soma andiko hili kwa makini, Utupe ni mda upi( yaani ni Present, Future, ao Past. inasema: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto AMEZALIWA, PRESENT tayari Mtoto huyo ameshazaliwa Jee! Yesu amezaliwa Nabii Isaya anawahubiria watu?!
TUMEPEWA PRESENT mtoto mwanamume; yaani kasha zaliwa Tumepewa Mtoto Mwanamume Kama kweli ni Yesu basi maandishi ya badilishwe (TUTAPEWA) mtoto mwanamume.......
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Jee! Uwezo wa Kifalme upo begani Mwake Yesu? Namuuliza Yesu jee! ni kweli? Mathayo:20:20-24
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Jee! Yesu wewe ni Mungu mwenye nguvu? Luka:8:46= Luka:22:43=Zaburi:138:3
Baba wa milele,
kwa imani ya Kikristo Yesu kafa, vipi awe baba wa milele? na maana yake ni Mtu asiye kufa wala kusinziya, yupo hai milele.
Mfalme wa amani. Jee! Yesu wewe ni Mfalme wa Amani? Yesu anasema hapana mimi si Mtu wa Amani; Mathayo: 10:34-36
Marufuku kumpa uungu Yesu
Unashangaa Yesu kufufua/kuhuisha wafu?
Biblia inasema:
1. Elisha alifufua mtoto aliyefariki. (2 Wafalme 4:35).
2. Maiti alifufuka kwa kuguswa na mifupa ya Elisha. (2 Wafalme 13:3:21).3. Ezekiel alifufua jeshi kubwa. (Ezekiel 37:10)
No comments:
Post a Comment