Weather

Tuesday, February 3, 2015

KAMA HUSIMAMISHI SWALA NA PEPO HUTOIONA


Tumesahau ya kwamba wenye kutupwa motoni wanatokana na
kuacha kusimamisha Swalah? Qur-aan Tukufu yatueleza (tafsiri):
{{"Ni kipi kilichokupelekeni Motoni?" Waseme: "Hatukuwa miongoni
mwa waliokuwa wakiswali…"}} [al-Muddaththir: 42-43]
Hadiyth ifuatayo inafafanua zaidi (tafsiri):
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘Anhu): hakika amesema
Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam): ((Umma wangu wote utaingia Peponi isipokuwa kwa
atakayekataa)) Pakasemwa: na ni nani huyo atakayekataa ewe
Mjumbe wa Allaah? Akasema: ((Mwenye kunitii mimi ataingia Peponi,
na atakayeniasi basi huyo amekataa)). [Imepokelewa na Al-Bukhaariy,
Buluughul-Maraami, Hadiyth ya 157]
Ila yahitajika juhudi na kuonesha moyo wa kumukhofu Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala). Tusitegemee tulale tuu halafu tushushiwe
riziki kama alivyofanyiwa bibi Maryam '(Radhiya Allaahu ‘Anha).

No comments:

Post a Comment