Weather

Tuesday, February 3, 2015

Tarahwih Sala ya Usiku


Kutoka kwa Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema, “ Alikuwa Mtume {Swalla Allahu alayhi wasallam} Akisali rakaa kumi na moja usiku (witri), na pale inapochomoza alfajiri husali rakaa mbili za hafifu(fupi) kisha hulala kwa ubavu wake wa kulia mpaka atakapokuja muadhini na kumjuza kuwa watu washafika kwa sala.”
{Imepokelewa na Bukhary na Muslim}
FAIDA NA MAFUNZO YA HADITHI
Mtume {Swalla Allahu alayhi Wasallam} anatufundisha kwa vitendo jinsi muislamu anatakiwa aweje katika kujipinda kiibada kwa kuamka na kusali kwa sala za sunna.
Kama Qur-an inavyotueleza {SURATUL MUZAMMIL 73:1-3} “Ewe uliyejifunika vazi! Simama usiku ila kidogo, Nusu yake au ipunguze kidogo,”
Mtume {Swalla Allahu alayhi Wasallam} akatekeleza amri hiyo na Allah akamthibitisha katika sura hiyo hiyo Aya ya 20 na ya mwisho aliposema “Kwa hakika Mola wako Anajua kuwa wewe husimama (kumwabudu) karibu na thuluthi mbili za usiku, pengine nusu yake, au thuluthi yake, na (pia) baadhi ya watu walio pamoja nawe; na Mwenyezi Mungu Huupima usiku na mchana………..”
Angalia Juhudi na kujipinda kwa Mtume {Swalla Allahu alayhi wasallam} kwa ajili ya ibada na kumuomba Mola wake kwa sala, japo Allah alishamsamehe madhambi yake yaliopita na yatakayokuja kama Suratul-Fathi {48:1-2} ilivyoanza “ Bila shaka Tumekupa ushindi uliodhahiri, Ili Mwenyezi Mungu Akufunikie makosa yako (unayosingiziwa) yaliyotangulia na yajayo, na kukutimizia neema Yake na kukuongoza katika njia iliyonyoka”
Mradi wake ni makosa ambayo makafiri na wanafiki walimsingizia, kama kuzua uwongo juu ya Mwenyezi Mungu au kukosa katika matendo mengine.
Ila hakuacha kumuabudu na kujipinda kwa Mola wake je mimi na wewe?
Tujitahidi kupata walau rakaa tatu za witri Amesema mwenye kusema “TANGULIZA KILE ANACHOKIPENDA MOLA WAKO {KUSALI KABLA YA KULALA} KABLA YA KUFANYA KILE UNACHOKIPENDA KATIKA NAFSI YAKO {KULALA}
WAFFAKANNALAHU FIYMAA YUHIBUHUU WAYARDHWAA.
 posted by Ally Glass

Nasaha za Luqmaan

Nasaha za Luqmaan Al Hakeem zilizokusanywa na wanazuoni akiwemo Ibn Kathir, ambazo hazimo katika Qur’an. Miongoni mwao ni:
1-Kuungana na watu wanaomkumbuka Allah na kujitenga na wale ambao wamemsahau Allah.
Kutoka kwa Damurah As-Sariy Ibn Yahia: Nimeambiwa na baba yangu kutoka kwa ‘Abdah Ibn Sulaymaan kutoka kwa Ibn Mubaraak kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan al Mas’uud kutoka kwa ‘Awn Ibn ‘Abdillaah akisema:’ ‘ Luqmaan alimwambia mwanawe: “Ewe mwanangu ukikutana na watu anza kwa salaam [Assalaamu ‘alaykum]. Kisha kaa upande na usiseme kitu hadi waseme wao. Ukiwaona wanamdhukuru Allaah, waunge, lakini wakishughulika na mengine, geuka uondoke mbali nao na tafuta wengineo [wanaomdhukuru Allaah].”
2-Kukaa kimya ni wingi wa kheri
‘Abdur-Razaaq amesema: Niliambiwa na Hasan kutoka kwa Al-Junayd kutoka kwa Sufyaan akisema: Luqmaan alimwambia mwanae: “Ewe mwanangu! Sijapata kujuta kwa sababu ya kukaa kimya.”
3-Hakuna kuchuma kuzuri kama kuchuma kwenye njia ya Allah.
Saiyar amesema: Niliambiwa na Ja’far kutoka kwa Malik Ibn Dinar akisema: “Luqmaan alisema kwa mwanawe, Ewe mwanangu, fanya biashara na Allah kwa kumtii, utapata faida bila ya kuhitaji bidhaa zozote.”

No comments:

Post a Comment